Miongozo hii inakusudiwa kukupa utangulizi wa haraka katika biashara ya kuendesha rilei yako wa kutoka.
KUMBUKA:
Maswali haya yanayoulizwa mara kwa mara ni ya madhumuni ya habari pekee na haijumuishi ushauri wa kisheria.
Lengo letu ni kutoa maelezo ya jumla ya maswala ya kisheria yanayozunguka uwasilishaji wa Tor ya kutoka.
Utofauti wa hali halisi na utofauti wa mamlaka kisheria hutoa majibu tofauti kwa maswali kadhaa.
Kwa hivyo, unaombwa usichukue hatua pekee yako na habari hii; ukiwa na tatizo lolote la kisheria, suala au maswali pata maelezo kamili kuhusu linalokukumba kutoka kwa wakili aliyesajiliwa kuhudumu kwenye eneo lako.
Mwenyeji
Tor kwenye vyuo vikuu: pata washirika.
Tafuta baadhi ya maprofesa (au wakuu wa vitivu!) wanaopenda la kuunga mkono na/au kutafiti kutojulikana kwenye mtandao.
Ikiwezekana, tumia anuwai ya ziada ya itifaki wa mtandao ambayo mawasiliano yake ya matumizi mabaya hayapitii timu kuu ya matumizi mabaya ya chuo kikuu.
Kikamilifu, tumia anwani ambazo haziaminiki na uthibitishaji wa msingi wa Itifaki wa mtandao hutumia huduma nyingi zinazohusiana na maktaba --ikiwa nafasi ya anwani ya itifaki wa mtandao wote wa chuo kikuu "inaaminika" kufikia rasilimali hizi za maktaba chuo kikuu kinalazimishwa kudumisha mtego wa nguvu kwenye anwani zake zote.
Pia soma Nawezaje kufanya chuo changu kikuu / ISP / nk kuwa na furaha na nodi yangu ya kutoka?
Tafuta watoa huduma wa mtandao walio marafiki wa Tor.
Mtoa huduma wa mtandao mzuri ni yule anayetoa kipimo data cha bei nafuu na haitumiwi na wanachama wengine wa jumuiya ya Tor.
Kabla ya kuendelea unaweza uliza jumuiya ya Tor kama chaguo lako ni zuri.
Tunahitaji anuwai sana, na haisaidii ikiwa tutakusanya njia nyingi za kutoka kwenye mtoa huduma wa mtandao mmoja wa kirafiki.
Kwa hali yoyote ile, ongeza mtoa huduma wa mtandao kwa kurasa ya GoodBadISPs.
To find an ISP, go through forums and sites where ISPs post their latest deals, and contact them about Tor hosting.
Once you have identified your ISP, you can follow the two-step advice of TorServers.net.
1.Uliza kama Mtoa huduma wa mtandao ako sawa na Tor ya kutoka
- Ikiwa watarudi na matumaini mazuri waulize ikiwa wako sawa na ugawaji upya wa safu ya Itifaki wa mtandao.
Kama sivyo, unaweza bado kueleza kuwa wewe ni shirika kubwa lisilo la faida lililojazwa na wataalamu wa usalama na kwamba yote yatakuwa sawa na kwa nini ugawaji upya wa Itifaki wa mtandao utasaidia kupunguza mzigo wao wa kazi.
The two-step process usually helps in elevating your request to higher levels of support staff without scaring them off too early, even if you don't end up with your own IP range. Here is a template you can use: Inquiry
Kisheria
Make sure you know the relevant legal paragraphs for common-carrier-like communication services in your country (and the country of your hosting provider!).
Angalau nchi nyingi za magharibi zinapaswa kuwa na kanuni ambazo zinawatenga watoa huduma ya mawasiliano kutoka kwa dhima.
Tafadhali ongeza kanuni za nchi yako kwenye orodha.
Ikiwa taifa lako halijajumuishwa hapa na unajua wakili anayeweza toa maoni ya kisheria tafadhali wasiliani na mradi wa Tor.
If you're part of an organization that will be running the exit relay (ISP, university, etc), consider teaching your legal people about Tor.
Ni bora zaidi kwao kusikia kuhusu Tor kutoka kwako katika mazingira tulivu kuliko kusikia kuihusu kutoka kwa mgeni kupitia simu. Wafahamishe Maswali Yanayoulizwa Mara kwa mara ya Kisheria ya Msingi wa mipaka ya kielektoniki kwa Waendeshaji Tor]. Msingi wa mpaka wa kielektroniki pia amejitolea kuzungumza na wanasheria wengine ili kuelezea vipengele vya kisheria vya Tor.
Kama wewe si sehemu la shirika fikiria kuanzisha moja!
Depending on the chosen form, setting up a legal body might help with liability, and in general, it helps to appear bigger than you are (and less likely to get raided).
Watu kutoka Torservers.net walio Ujerumani walipata wakili aliyekubali kuwa "mwenyeji" wao ndani ya ofisi yake.
They are now a non-profit association ("eingetragener Verein, gemeinnutzig") registered inside a lawyer's office.
Mchakato wa usanidi ulikuwa rahisi na wa bei nafuu. Mipangilio kama hiyo huenda ipo kwa ajili ya nchi yako.
Faida nyingine ya muundo kama ule wa shirika ni kuwa utaweza kufanya kazi hata ukiondoka ikiwa utaweza kupata warithi.
Zingatia kufundisha kwa uangalifu wanasheria wa eneo lako kuhusu Tor.
"Uhalifu wa Mtandao" watu hupenda sana unapojitolea kuwafundisha kuhusu Tor na Mtandao -- kwa kawaida wanalemewa na kazi zao na hawana historia ya kutosha kujua waanzie wapi.
Kuwasiliana nao inakupa nafasi ya kuwafunza mbona Tor ni muhimu kwa ulimwengu (na mbona ni haina msaada yoyote kwa wahalifu).
Pia, ikiwa watapata ripoti kuhusu rilei yako watakufikiria kama mtaalamu anayesaidia badala ya mhalifu.
Kushughulikia malalamiko ya unyanyasaji
Kujibu malalamishi
Ukipokea malalamiko ya unyanyasaji usifadhaike! Hii hapa ni ushauri kwako:
Jibu malalamiko ya unyanyasaji kwa njia ya kitaaluma ndani ya muda unaofaa.
TorServers.net is a fairly large Tor exit operator, and we receive only a very small number of complaints, especially compared to the amount of traffic we push.
Takriban 80% ni ripoti za kiotoamatiki na zilizosalia kwa kawaida huridhishwa na jibu letu la chaguomsingi.
Hatujahitaji maoni ya wakili katika miaka mingi ya operesheni kufuatia ushauri kwenye ukurasa huu.
Pamoja na violezo vya Torservers.net unaweza pata violezo vingi zaidi vya matukio mbalimbali yaviolezo vya matumizi mabaya ya Tor.
Ni nadra sana kukumbana na hali ambapo hakuna violezo vyovyote vinavyoweza kutumika.
Ukipokea barua ya vitisho kutoka kwa wakili kuhusu matumizi mabaya au malalamiko ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali, pia usifadhaike.
Hatujui kesi yoyote iliyofikia karibu na mahakama na tutafanya kila tuwezalo kadri ya nguvu zetu kukusaidia ikiwa itafanyika hivyo.
Unaweza angalia kama anwani ya itifaki ya mtandao iliyoorodheshwa na rilei ya kutoka kwa wakati wowote ExoneraTor. Ashiria kwa tovuti hiyo kwa jibu lako la malalamiko.
Ikiwa unahisi itaweza kusaidia, tunaweza kukuandikia barua iliyotiwa sahihi kuthibitisha taarifa hii: Wasiliana nasi kwa frontdesk@torproject.org ikiwa unahitaji moja.
Kwa jibu lako, sema kwa uwazi kuwa hauna wajibu kwa maudhui yaliyotumwa kupita kwenye mashine yako na kujumuisha marejeleo ya kisheria yanayofaa kwa nchi yako.
Mambo unayoweza fanya bila kutarajia
Weka maelezo ya WHOIS karibu nawe iwezekanavyo.
Moja ya sababu kubwa ya rilei za kutoka kutoweka ni kwa sababu watu wanaojibu anwani ya matumimizi mabaya hupata woga na kukuuliza uache.
Ukiweza kupata bloku yako ya Itifaki wa mtandao, hiyo ni nzuri. Hata kama sivyo, watoa huduma wengi bado watakukabidhi bloku ndogo ukiuliza.
ARIN hutumia SWIP na RIPE hutumia kipengee kama hicho.
You can also add comments to your range, hinting at your usage as an anonymization service (Example).
Ikiwa una maswali kuhusu mchakato tafadhali andika barua pepe kwa orodha ya barua pepe ya rilei za tor na tutajaribu kueleza mchakato huo kwako.
Sajili nambari ya simu na nambari ya faksi kama anwani yako ya matumizi mabaya.
Angalau utekelezaji sheria nchini Ujerumani hutumia mara kwa mara nambari za faksi na simu zilizopo kwenye rekodi ya itifaki ya mtandao.
Torservers.net hutumia huduma ya bure faksi -kwenda kwa-barua pepe kutoka Ujerumani, call-manager.de na nambari ya VoIP kutoka Sipgate.de.
Zingatia kutumia sera ya kutoka iliyopunguzwa.
Sera ya kutoka iliyopunguzwa ni mbadala wa sera chaguomsingi ya kutoka.Inaruhusu huduma nyingi za Mtandao huku bado inazuia port nyingi za TCP.
Hii inapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano kwamba mtumiaji wa Bittorrent atachagua nodi yako na hivyo kupunguza au hata kuondoa idadi ya malalamiko ya DMCAutakayopokea.
Ikiwa una uzoefu wako mwenyewe wa kushughulikia unyanyasaji uishiriki tu kwenye orodha yetu ya barua pepe ya umma au utuandikie barua pepe kwa frontdesk@torproject.org.
Kiufundi
Tafadhali soma maelezo yote ya kiufundi kabla ya kuanza. Ikiwa una maswali yoyote au unahitaji msaada, tafadhali wasiliana nasi kwa rilei za tor.
A disclaimer helps give people the right idea about what is behind the traffic coming from these IPs.
Notisi rahisi inaweza kuchapishwa bila seva ya tovuti tofauti kwa kutumia mwongozo wa Tor "DirPortFrontPage".
Try to use dedicated IPs, and when possible, dedicated hardware.
Disk encryption might be useful to protect your node keys, but on the other hand, unencrypted machines are easier to "audit" if required. We feel it's best to be able to easily show that you do Tor exiting, and nothing else (on that IP or server).
Weka DNS kinyume kwa kitu kinachoashiria matumizi yake, k.m. 'rilei isiyojulikana', 'proksi', 'proksi ya tor'. Kwa hivyo watu wengine wanapoona anwani kwenye kumbukumbu zao za wavuti, wataelewa kwa haraka zaidi kinachoendelea.
Ukifanya hivyo, na ikiwa SMTP inaruhusiwa katika sera yako ya kuondoka zingatia kusanidi SPFkwenye kikoa chako: hii itakulinda dhidi ya watumiaji wanaotumia njia yako ya kutoka kuunda barua pepe ambazo zinaonekana kama zinatoka kwako.