Imeandikwa na Msingi wa Mpaka wa Kielektroniki (EFF). Ilisasishwa mwisho Machi 27, 2020.
Barua kwa waendeshaji wa rilei za Tor: katika enzi hii ya madai, mtu yeyote anayetoa huduma ya uelekezaji anaweza kukabiliwa na malalamiko ya hakimiliki kwa yaliyopitishwa.
Kwa bahati, sheria ya hakimilki inafaa kutoa ulinzi kutokana na mingi ya hizi vitu kwako na pia kwa wahudumu juu yako.
Kama mwenyeji wako wa mtandao anakuletea malalamiko ya hakimiliki, unaweza tumia kiolezo hiki kuandika jibu ingawa utahitaji kugeuza kufaa hali yako.
Tafadhali hakikisha kwamba kauli zote ni kweli kwako.
Mradi wa Tor una kigezo cha mkusanyiko wa unyanyasaji] kukusaidia kujibu aina zingine za malalimiko ya unyanyasaji pia)
Kabla ya kutuma jibu lolote kwa mtoa hudumu ya mtandao yako, unaweza jaribu kutafuta ushauri kutoka kwa wakili aliyesajiliwa kudumu katika eneo lako.
Kiolezo hichi cha barua kwa taarifa maalum pekee na sio cha kuunda ushauri wa kisheria.
Iwapo na jinsi unavyopaswa kujibu wakati wewe au ISP wako anapopokea notisi ya hatimiliki itaamsha ukweli mahsusi wa hali yako.
Kiolezo hiki kimekusudiwa kama hatua ya kuanzia, lakini unapaswa kuirekebisha kulingana na hali yako mwenyewe.
Zaidi ya hayo, ni juu yako kuzungatia masharti ya huduma ya mtoa wa huduma wa mtandao wako.
Kama hujaridhika ikijumuisha maelezo mengi ya kisheria, jihisi huru kualika mtoa huduma wa mtandao azungumze na Msingi wa Mpaka wa KIelektroniki kwa mjadala kamili.
Kama umepokea hii hati kutoka mahali popote isipokuwa tovuti ya EFF ama tor-dmca-response, itakuwa imepitwa na wakati.
Fuata kiungo hiki ili kupata tafsiri jipya.
Mpendwa [Mtoa Hudumu ya Mtandao]:
Asante kwa kunisambazia notisi umepokea kutoka[mdai hakimiliki] kuhusu [yaliyomo]. Ningependa kukuhakikishia kuwa mimi si mwenyeji wa nyenzo zinazodaiwa si za haki, Sheria ya Hakimiliki ya Milenia ya Kidigitali hifadhi salama inakukinga dhidi ya dhima ya madai inayotokea. Notisi hii yaweza kuwa inalingana na kutoeleweka kwa sheria na kuhusu baadhi ya programu ninayoendesha.
Unavyojua, Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali hubuni hifadhi nne salama ya watoa hudumu kuwalinda kutokana na dhima ya hakimilki ya watumizi wao wakati mtoa huduma ya mtandao ameafikia masharti fulani.(17 U.S.C. 512)
Mahitaji ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki ya Kidigitali inabadilika kutegemea na jukumu la mtoa huduma za mtandao wako.Unaweza kuwa na fahamu kuhusu masharti ya "ilani na kuondoa" ya kifungu cha 512(c) cha Sheria ya Milenia ya Hakimiliki ya Kidigitali; hata hivyo, hizo hazitumiki wakati mtoa huduma za mtandao anafanya kazi kama mfereji.
Badala yake, "mfereji" wa hifadhi salama sehemu 512(a) ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki ya Kidigitali ina mahitaji tofauti na yenye mzigo mdogo wa kustahiki, jinsi mahakama ya rufaa ya sakiti ya D.C. iliyofanyika RIAA v.(tazama https://scholar.google.com/scholar_case?case=15815830240179540527) na sakiti ya rufaa pale RIAA v. Mkataba (tazama https://scholar.google.com/scholar_case?case=11547531128234336420).
Chini ya DMCA 512(a), watoa huduma kama wewe kwa kawaida hulindwa dhidi ya uharibifu wa madai wa ukiukwaji hatimiliki ikiwa pia inadumisha "sera inayoruhusu kusitishwa kwa hali zinazofaa za waliojisajili na wamiliki wa akaunti za mfumo wa watoa huduma au mtandao unaorudia ukiukwaji."
Ikiwa unayo na unatekeleza sera kama hiyo unahitimu vinginevyo kwa hifadhi salama, uko huru kutoka na hofu ya madhara ya hakimiliki.
Notisi ya hakimiliki uliyopokea inawezekana iliyosababishwa na programu uliyoendesha inayoitwa Tor. Tor ni programu ya mtandao inayosaidia watumizi kuimarisha faragha, usalama na kinga mtandaoni.
Haipangishi maudhui yoyote. Badala yake ni sehemu ya mfumo mtandao wa nodi kwenye mtandao ambayo kwa urahisi unapitisha pakiti miongoni mwa kabla ya kuzituma zinapotarajiwa kuenda mwishoni, kama vile mtandao wa suluhishi kati hufanya.
Tofauti ni kwamba Tor huunganisha miunganisho hivi kwamba hakuna hop inayoweza kujifunza chanzo na mwisho wa pakiti, hivyo kuwapa watumiaji ulinzi dhidi ya upepekezi mbaya kwenye trafiki ya mtandao.
Matokeo ni kuwa tofauti na trafiki nyingine nyingi za mtandao, anwani ya mwisho ya IP anayoipokea mpokeaji sio anwani ya mwisho ya IP ya mtumaji.
Tor hulinda watumiaji wake dhidi ya hatari kama vile unyanyasaji, barua taka, na kutambua wizi. Maendeleo ya awali ya Tor, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa mtandao wa Tor kwa matumizi ya umma, ulikuwa mradi wa U.S. Naval Research Laboratory, kwa ufadhili kutoka ONR na DARPA. (Kwa zaidi kuhusu Tor, angalia https://decvnxytmk.oedi.net/.)
Natumai kama shirika linalojitolea kukinga faragha ya wateja wake, utakubaliana nasi kuwa hii ni teknolojia yenye thamana.
Wakati ninapoendesha nodi ya Tor inayoonekana kuwa chanzo cha nyenzo inayodaiwa kukiuka hakimiliki, mimi si mwenyeji wa nyenzo hiyo.
Sichagui nyenzo inayotangazwa kupitia nodi ya Tor ninayoendesha sina pia njia ya vitendo ya kutambua chanzo cha nyenzo au kuzuia utangazaji.
Sifanyi chochote kuhimiza au kukuza utumizi wa mtandao wa Tor kwa ukiukaji wa hakimiliki.
Kwa sababu hizi, mimi si mhalifu wa hakimiliki kwa nyenzo inayopitishwa na nodi ya Tor ambayo ninaendesha iwe ni moja kwa moja au chini ya nadharia ya kusaidia uchangiaji au lililotendwa kwa niaba ya dhima.
Kwa hiyo, unapaswa kuendelea kulindwa chini ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki ya Kidigitali 512(a) hifadhi salama bila kuchukua hatua yoyote zaidi.
Asante kwa kufanya kazi nami kwa suala hili. Kama mteja mwaminifu nashukuru kwa kunijulisha kuhusu suala hili na ninatumai kwamba ulinzi wa Sheria ya Millenia ya Hakimiliki ya Kidigitali 512 utaondoa mashaka yoyote ambayo unaweza kuwa nayo.
La sivyo, tafadhali wasiliana nami na maswali yoyote zaidi.
Kweli kabisa wako,
Mteja wako,[mtumiaji]